Kila siku mimi huamka saa kumi na mbili na dakika arobaini asubuhi. Kwanza hufanya mazoezi kidogo, kisha huoga, hupiga mswaki na hunyoa ndevu. Baada ya hapo huvaa nguo na hunywa chai ya asubuhi. Kawaida hula nafaka (CornFlakes) na mayai. Mimi hunywa chai.
Mimi hujaribu kuacha nyumba kabla ya saa mbili asubuhi. Mimi huenda kazini kwa gari. Kawaida mimi hufika kazini saa tatu asubuhi. Kazini mimi hunywa vikombe vingi vya kahawa.
Mimi humaliza kazi saa kumi na moja mchana. Mimi hurudi nyumbani, kisha huenda kwenye sehemu ya mazoezi. Hurudi kutoka mazoezi saa mbili unusu usiku. Baada ya hapo mimi huoga. Kisha hula chakula cha jioni. Baada ya hapo mimi hulala.
Sunday, September 14, 2008
Subscribe to:
Posts (Atom)